Makontena
mengine 11884 pamoja na magari 2019 yamebainika kuwa yametolewa
katika bandari ya Dar es salaam bila kufuata taratibu za ulipaji wa
kodi na kulikosesha taifa mapato ya zaidi ya shilingi bilioni 49 na
kuwataka wahusika walipe fedha hizo haraka iwezekanavyo kabla ya
kuchukuliwa hatua za kisheria.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa amesema hayo
jana jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa ukwepaji huo wa kodi
ulifanywa na bandari kavu zinahusika na makontena na bandari kavu
zinazohusika na uingizaji wa magari huku akiwataka waliolipa
wawakilishe vielelezo vyao.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa
Prof.
Mbarawa amesema kuwa kutokana na sakata hilo watumishi 7 wa mamlaka
ya bandari wanaohusika na bandari kavu za makontena na magari
wamekamatwa na kufikishwa katika vituo vya polisi kwa hatua zaidi za
kisheria huku wengine nane wakitafutwa.
Desemba
7 mwaka huu waziri mkuu Kasim Majaliwa alitangaza upotevu wa
makontena 2431 katika bandari kavu nne za Azam,DICD,JEFAG na PMM
ambapo safari hii bandari kavu hizo nne zimehusika tena na upotevu na
makontena hayo mengine.

No comments:
Post a Comment