Waziri
wa Maliasili na Utalii Pro. Jumanne Maghembe amemsimamisha kazi
Mkurugenzi wa mipango na matumizi ya rasilimali wa wakala wa misitu
nchini Mohamed Kilongo.
Waziri
Maghembe amechukuwa hatua hiyo leo baada ya kugundua uzembe katika
usimamizi wa rasilimali za wakala hao wa misitu ikiwa ni pamoja na
Mkurugenzi huyo kushindwa kuwasimamia maafisa maduhuli ambao
wameshindwa kukusanya na kuwasilisha maduhuli ya serikali kwa wakati.
Aidha
Pro. Maghembe ameagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa serikali (CAG),
kupitia upya vitabu vyote vya mapato ya wakala huo wa misitu nchini
kwani takwimu zinaonesha kuwa kuna maafisa maduhuli hawajawasilisha
fedha za serikali toka mwaka 2004.
Wakati
huo huo Waziri Maghembe amewataka maafisa wa wakala wa misitu
waliopanga ofisi nje ya jengo la wakala wa misitu la Mpingo House
warudi haraka katika jengo hilo ndani ya siku 7 zijazo pamoja na
kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kuipa hasara serikali.
No comments:
Post a Comment