Serikali
imeliagiza jeshi la polisi na Taasisi ya kuzuia na kupambana na
rushwa kuwakamata, kuwahoji na kuwafikisha mahakamani viongozi na
watendaji wote hata kama wamestaafu madaraka yao, walio husika kutoa
shamba la ukubwa wa zaidi ya hekari 3,500, katika kijiji cha
mlilingwa wilayani morogoro,.
Agizo
hilo limetolewa na waziri wa Ardhi, Nyumba na maendeleo ya makazi,
William Lukuvi ,baada ya kutembelea kijiji hicho cha
Mlilingwa,Ngerengere, kwa lengo la kujiridhisha juu ya mwenendo mzima
wa utoaji wa eneo hilo ambao ulitiliwa mashaka na rais.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Willium Lukuvi akiongea na wananchi wa Kijiji cha Mlilingwa.
Mhe.
Lukuvi amelazimika kukagua sahihi za wana kijiji walio orodheshwa
majina yao ambapo wengi wa waliohojiwa wamezikana sahihi hizo na
kueleza kushangazwa na hali hiyo na hata baadhi ya majina
yaliyotumika ambayo sio ya wanakijiji wenzao na kudai katika kikao
hicho hakuna mwenyekiti mjumbe wala mtendaji aliyekua kwenye sakata
hilo aliyeudhuria kikao hicho.
Wananchi wa Kijiji cha Mlilingwa wakimsikiliza waziri Lukuvi kwa umakini
Mwakilishi
wa kampuni ya Oxfod TradingLTD aliyehudhuria mkutano huo wa kijiji,
ameonekana kushindwa kujieleza vyema pale alipokuwa akihojiwa
maswali kwa madai bado ni mgeni katika kampuni hiyo na hakuwepo
wakati wa mkutano wa kuidhinisha kutolewa kwa eneo hilo,
Baada
ya kujiridhisha, Waziri Lukuvi ameagiza mtu huyo kukamatwa na ofisa
wa polisi ili kusaidia kukamatwa kwa wahusika wote wa sakata hilo na
kuagiza uchunguzi pia kufanywa kwenye ofisi zote ili watakaobainika
kuhusika na udanganyifu huo wafikishwe mahakamani
Waziri
lukuvi amesema zoezi hilo litakua endelevu nchi nzima hivyo
kutahadharisha kama kuna mwekezaji yeyote aliyejipatia ardhi kwa njia
ya udanganyifu bila kufuata taratibu, ni vyema akaanza upya kufuata
maagizo ya serikali,na ikibainika kuna kosa popote shamba lake
litafutiwa milki yake na kubadilishwa matumizi kwa mujibu wa
sheria.
No comments:
Post a Comment