Shirikisho
la Wafanyakazi nchini Tanzania (TUCTA),limetiaka serikali kuongfeza
juhudi katika upekuzi wa viwandani na sehemu nyinginezo za uzalishaji
kwa kuwa wageni wengi wasio na vibali inasemakana wanafanya kazi
huko.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa
Shirikisho la Wafanyakazi, Nicolas Mgaya amesema wamebaini wageni
wengi wanfanya kazi kwa kujificha katika viwanda mbalimbali nchini
kwa kufanya kazi mchana na kutoka usiku.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Wafanyakazi, Nicolas Mgaya
Mgaya
amesema ili fursa za ajira ziongezeke nchini srikali haina budi
kupita kiwanda kwa kiwanda nyumba kwa nyumba ili kuwabaini
wafanyakazi raia wa Kigeni wanaofanyakazi kinyume cha sheria.
Aidha
Mgaya ameongeza kuwa kwa sekta nyingi za uzalishaji ikiwemo na
mahoteli zimevamia na rais wa kigeni kutoka nchi jirani na kufanya
shughuli ambazo hata watanzania wengine wa kawaida wana uwezo wa
kuzifanya.

No comments:
Post a Comment