Breaking News
recent

Serikali imetoa karipio kali kwa wafanyabishara wa sukari nchini wanaoficha sukari

Serikali imetoa karipio kali kwa wafanyabishara wa sukari nchini wanaoficha sukari katika maghala yao ya sukari na kusema haita sita kuwafungia watakaobainika.

Akizungumza na waaandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Charles Mwijage amawataka wadau wakiwemo wananchi wanaowafahamu wafanyabishara wanaoficha sukari wawafichue ili wawashughulikie.
              Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Charles Mwijage 
Mhe. Charles amesema kwa taarifa ambazo serikali inazo mpaka sasa hakuna upungufu wowote wa sukari na kusema mfanyabiashara atakaebainika kufucha sukari serikali haitasika kuwafutia leseni zao.


Katika hatua Nyingine Waziri huyo wa viwanda amesema katika mchakato wa kufufua viwanda serikali imepanga kukirejesha kiwanda cha General tyre na yatari serikali imekwisha chukua hisa aslimia mia moja na wako mbioni kuanza uzalishaji.
gmbongo tha entertainer

gmbongo tha entertainer

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.