Ukamilishaji wa Mahakama
itakayowashughulikia mafisadi umeanza baada ya rais John Magufuli
kutoa ahadi kwa wananchi wakati wa kampeni kuwa atafungua mahakama
hiyo itakayowashughulikia wale wote wanajihususha na ufisadi na
vitendo vya rushwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe amesema wamepiga hatua kubwa katika ukamilishaji wa mahakama hiyo wananchi wasubiri kauli ya serikali lini mahakama hiyo itafunguliwa.
Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Dkt. Harrison Mwakyembe
Mhe Mwakyembe amesema kuwa kazi ya msingi ya kukamilisha uanzishwaji wa mahakama hiyo imeshakamilika kilichobaki ni kuepeleka vyombo vya juu zaiidi ili iweze kupata baraka huku akibainisha kuwa katika kufanikisha hilo wamemshirikisha Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba.
Akizungumza juu ya uboreshaji wa Mahakama hiyo waziri huyo Mkuu Mstaafu ambae pia aliwahi kuwa waziri wa Katiba na Sheria amesema kuwa uanzishwaji wa Mahakama hiyo haitoshi bila kuboresha vyombo vinavyoshirikiana katika endeshaji wa Kesi.
Jaji Wairoba amesema kuwa suala la uanzishwaji wa Mahakama hiyo ni jambo zuri lakini chimbo kimoja hakiwezi kushughulika tatizo hilo pekee yake bila ya kuwepo ushiriki mzuri wa Jeshi la Polisi naTakukuru ambao wanahusika moja kwa moja.

No comments:
Post a Comment