Mwenyekiti
wa zamani wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba amesema
kuwa hausiki na vurugu zilizoibuka katika mkutano mkuu wa chama hicho
uliovunjika juzi wakati wa uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi.
Akitoa
ufafanuzi huo jana Jijini Dar es Salaam, Prof. Lipumba amekiri ni
kweli hakualikwa katika mkutano huo lakini aliombwa na baadhi ya
wajumbe kwenda kutoa maelezo ya kwanini aliachia nafasi hiyo ya
uenyekiti jambo ambalo viongozi waliokuwepo ukumbini hapo
hawakulitaka.
Mwenyekiti wa zamani wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba
Prof.
Lipumba amesema kuwa anaheshimu maamuzi ya pande zote mbili kwa
wanaomtaka arejee nafasi ya uenyekiti lakini pia maamuzi ya chama
endapo utaratibu utafuatwa kwa kufuata katiba ya chama na demokrasia
ya kweli ndani ya chama hicho.
Prof.
Lipumba amekata kuhusika kukana kutumika na kisiasa na baadhi ya watu
ili kukivuruga chama hicho na kusema kuwa viongozi wa chama hicho
waepuke maneno ambayo yataweza kukigawanya chama hicho na badala yake
wakijikite katika kudumisha demokrasia ndani ya chama hicho.

No comments:
Post a Comment