Kamati
ya ulinzi na usalama mkoani Morogoro wamesitisha rasmi zoezi la
ubomoaji wa nyumba lililokua likifanyika katika eneo la CCT Forest
kata ya Mkundi katika manispaa hiyo baada ya kuibuka hali ya
sintofahamu kwa baadhi ya nyumba kubomolewa kwa madai zimo ndani ya
eneo la hifadhi ya msitu.
wakizungumza
na wananchi wa eneo hilo baada ya kutangazwa rasmi na serikali
kusitishwa kwa zoezi hilo,Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdulaziz
Abood amesema hawatakuwa tayari kuona kiongozi yeyote wa serikali
anasababisha migogoro kama iliyojitokeza katika eneo la hilo kwakuwa
imesababisha hasara na usumbufu mkubwa na kimewafanya wananchi
kupoteza imani na serikali yao.
Mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdulaziz Abood
Mh.
Abood ameongeza kuwa hawatamvumilia mtu yeyote atakaye rudisha
migogoro ya aina hiyo huku Diwani wa kata ya mkundi Hilda Benedict
akiwasihi wananchi kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki wakati
wakishugulikia maswala ya malipo ya fidia kwa nyumba 15 zilizo kwisha
vunjwa.
No comments:
Post a Comment