Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amewashukuru Viongozi na Waumini wa Kanisa la Anglikana na Madhehebu
mengine ya Dini hapa nchini kwa kuendelea kuliombea Taifa na
kudumisha amani na utulivu.
Rais
Magufuli amezingumza hayo mara baada ya baada ya kumalizika kwa
Ibada,katika kanisa la Angilikana la Mtakatifu Albano lilipo Jijini
Dar es salaam ambapo Rais Magufuli aliyeongozana na Mkewe Mama
Janeth Magufuli.
Dkt.
Magufuli amesisitiza kuwa Viongozi wa Dini wanafanya kazi kubwa na
muhimu katika Taifa na kwamba Watanzania wote bila kujali dini zao,
itikadi za kisiasa, makundi na kanda zao wana wajibu wa kuungana na
Viongozi hao ili nia hiyo njema iendelee kufanikiwa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
“Ninawashukuru
kwa sababu mnaendelea kuliombea Taifa hili, ninawashukuru kwa sababu
siku zote mmekuwa mkipiga magoti na kumtanguliza Mungu mbele,
ninawashukuru kwa sababu mnaendelea kuombea amani ya nchi yetu na
upendo udumu ndani yetu sisi sote.
“Makanisa
yote, Madhehebu yote, Dini zote, Vyama vyote, upendo tukiujenga ndio
tutaiendeleza vizuri Tanzania yetu” Amesema Rais Magufuli.
Kwa
upande wake Padre Jackson Sostenes aliyeongoza Ibada hiyo amemshukuru
Rais Magufuli kwa kuungana na waumini wa Kanisa hilo katika Ibada ya
Jumapili na ameahidi kuwa Viongozi na Waumini wa Kanisa hilo
wataendelea kumuombea na kuliombea Taifa.
Katika
Ibada hiyo Rais Magufuli ametoa Shilingi Milioni 1 kuchangia vikundi
vya kwaya vya kanisa hilo.
No comments:
Post a Comment