Mchungaji
wa kanisa la Evangelist Assemblies of God Tanzania (EAGT) katika
kijiji cha Mgongoro kata ya Igunga mkoani Tabora, Abel Godfrey,
amekamatwa na waumini wake baada ya kudaiwa kukutwa akifanya mapenzi
na binti wa kaka yake.
Waumini
hao wakishirikiana na uongozi wa serikali ya kijiji hicho, walifanya
tukio hilo juzi saa 5:30 usiku akiwa na binti huyo Magreth Emmanuel
(20) mwenye mtoto mchanga wa miezi minne.
Akizungumza
kwa masikitiko babu wa binti huyo, Bictoni Kyarero, alisema mchungaji
Godfrey, alikuwa na tabia hiyo kwa mwaka mmoja sasa, lakini tabia
hiyo ilimchosha na kutoa taarifa kwa waumini wake pamoja na uongozi
wa mtaa kisha kumuwekea mtego uliomnasa akiwa katika nyumba hiyo.
Picha ya kanisa lakini haihusiani na hii story
Amesema
baada ya kumkamata alijaribu kukimbia lakini walifanikiwa kumdhibiti
na kisha kukiri kufanya mapenzi na binti huyo huku akiwabembeleza
waumini wake wamfichie siri.
Kwa
upande wake binti huyo alipoulizwa kuhusu kufanya uzinzi na baba yake
mdogo, alikiri huku akisema alitenda kosa hilo baada ya kutishwa na
mchungaji huyo iwapo angekataa angemuombea kwa Mungu ili awe kichaa.
Akizungumzia
tukio hilo, mchungaji huyo amekiri kutenda kosa hilo na kubainisha
alifanya hivyo baada ya kuzidiwa ‘ujanja’ na shetani huku akitubu
na kudai hatorudia tena kosa hilo.
Naye
mtendaji wa kijiji hicho, Edward Kitenya, alisema mchungaji huyo
walimkamata akiwa katika nyumba ya tembe wakiwa wamelala baada ya
kutandika turubai chini wakiendelea kufanya mapenzi na binti huyo
kisha kumweka chini ya ulinzi mpaka asubuhi na kupigishwa faini ya
Sh. 20,000 na kuachiwa huru.
Kwa
upande wao baadhi ya wananchi waliuomba uongozi wa kanisa hilo kumvua
uongozi kwa kuwa amekiuka maadili ya uongozi na kufanya waumini
kutomwamini tena kama kiongozi wa kiroho.
Mtendaji
wa kata ya Igunga, Fredrick Masesa, amewaomba viongozi wa dini pamoja
na wananchi kwa ujumla kuzingatia maandiko matakatifu ya mwenyezi
Mungu ya kutofanya vitendo viovu ili wamtumikie kiusahihi.
Kwa
upande wake mchungaji wa kanisa la kijiji cha Mwanzugi, Fanuel
Daniel, alithibitisha kukamatwa kwa mchungaji wa kanisa la kijiji cha
Mgongoro, Godfrey na kusema tayari wamemsimamisha kutoa huduma
mchungaji huyo kwa muda usiojulikana mpaka uongozi utakapokutana wote
kwa ujumla na kuongeza kuanzia sasa kanisa hilo la Mgongoro
litaongozwa na Philipo Makeremo ambaye pia ni katibu wa kanisa.
No comments:
Post a Comment