Serikali
kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI), inaendesha mafunzo kwa walimu wa shule za sekondari
katika mikoa ya Lindi na Mtwara kwa ajili ya kuwajengea uwezo katika
masomo ya Hisabati, Baiolojia, Kiswahili na Kiingereza.
Akizungumza
katika mafunzo hayo, afisa elimu kutoka idara ya usimamizi wa elimu
ofisi ya Rais TAMISEMI Dodoma, Hellen Msellem, ambaye pia ni mratibu
wa mafunzo hayo, amesema mafunzo hayo yamewekwa mahususi kwa ajili ya
kuinua kiwango cha ufaulu katika masomo hayo ambayo katika miaka
mitatu iliyopita wanafunzi walionekana kuto fanya vizuri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh. George Simbachawene
Amesema,
kutokana na mwaka huu kiwango cha ufaulu kuwa ni asilimia 80,
imewekwa mikakati itakayowawezesha walimu na wanafunzi kufikia
malengo, ambapo miongoni mwake ni pamoja na huo wa kutoa mafunzo kwa
baadhi ya walimu ili na wao waende kuwafundisha walimu wengine.
Aidha,
baadhi ya walimu wanaoshiriki mafunzo hayo, wameiomba serikali kuto
ishia katika masomo hayo manne pekee, isipokuwa mpango huo uendelee
katika masomo mengine kwani kwa kufanya ivyo itasaidia kwa kiasi
kukubwa kuondoa tatizo la kufeli kwa wanafunzi wengi hapa nchini.
No comments:
Post a Comment