Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani
Mwanza Baraka Konisaga amewasimamsiha kazi watumishi wa tano wa
hospitali ya Butimba wilayani humo waliokua zamu ili kupisha
uchunguzi wa tuhumza za kusababisha vifo vya watoto wawili mapacha
vilivyotokea wakati mama watoto akijifungua.
Konisaga ametoa agizo hilo baada ya
watoto hao kufariki dunia baada ya mama yao Suzan John Mkazi wa
Jijini Mwanza kulazimika kujifungua kwenye beseni kufatia kukosa
huduma baada ya wauguzi waliokua zamu kushindwa kumsaidia.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Baraka Konisaga
Akielezea tukio hilo mama wa Watoto
hao marehemu Bi.Suzan John amesema kuwa baada ya kuzidiwa na kutaka
huduma wauguzi wa waliokua zamu kila alipowaita walikua wanamuangalia
na kuondoka na hali ilivyokua mbaya kwa msaada wa dada yake
alilazimika kujifungua kwenye Beseni.
Mkasa huo ulisababisha hali ya
Taharuki miongoni mwa Wananchi hususani wakinamama walioandamana
hospitalini hapo na hivyo kulilazimu Jeshi la Polisi wilayani
Nyamagana kuingilia kati huku wakina mama hao wakishusha lawama kwa
watumishi wa Hospitali hiyo.
Baada ya Sakata hilo Mkuu wa Wilaya
hiyo Bw. Baraka Konisaga alikutana na Uongozi wa Wilaya hiyo na
kupata maelezo ya jinsi ya tukio lilivyotokea ndipo alipoamuru
watumishi watano waliokuwa zamu kisimamishwa kazi ili kupisha
uchunguzi zaidi.
Watumishi waliosimamishwa kazi ni
Wauguzi Suzana Singama, Bibi Ana Moshi, na Janeth Foya, pamoja na Madaktari wawili Maureen
Magesa pamoja na Emiliana Mvungi.

No comments:
Post a Comment