Breaking News
recent

Serikali yaitaka Hospitali ya Aga Khan kuangalia upya gharama zake



Serikali imeutaka Mtandao wa Maendeleo wa Aga Khan (AKDN), ufanye mapitio ya gharama za afya katika hospitali ya Aga Khan ili wananchi wa kawaida waweze kumudu na kunufaika na huduma za tiba wanazozitoa.



Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi wa awamu ya pili ya upanuzi wa hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa pamoja na jitihada za Serikali za kuboresha huduma za afya, pia inatambua mchango unaotolewa na taasisi zisizo za Kiserikali ikiwemo Hospitali ya Aga Khan katika kuimarisha upatikanaji wa huduma za kisasa.



Amesema upanuzi wa hospitali hiyo ni miongoni mwa jitihada za kuwafikishia Watanzania huduma za afya katika maeneo yao na kwa ngazi zote na kwa gharama nafuu, hivyo amewataka watoa huduma wote nchini waangalie upya gharama zinazotozwa katika huduma mbalimbali hususan za matibabu.
gmbongo tha entertainer

gmbongo tha entertainer

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.