Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali haijaridhia viwango vipya vya
nauli ya mabasi yaendayo kasi vilivyopendekezwa na waendeshaji wa
huduma ya mabasi yaendayo kasi Dar es salaam (UDART).
Akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kuwasili katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam
akitokea mkoani Ruvuma kwa ziara ya siku 3, Waziri Mkuu amesema
Serikali haijaridhia viwango vipya vya nauli ya mabasi yaendayo kasi.
Ambapo nauli ya kutoka Mbezi hadi Kimara shilingi 700, Mbezi hadi
Kariakoo shilingi 1200, na nauli ya kutoka Mbezi hadi Mwenge shilingi
1400 na wanafunzi watatozwa nusu ya viwango hivyo vya nauli.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Waziri
Mkuu amesema gharama hizi ni kubwa mno kwa wananchi na watumishi,
mradi ulilenga kumrahisishia mtumishi wa Serikali anayeishi nje ya
jiji, “Serikali iliwekeza katika mradi huu ili kusaidia watumishi
na wananchi ambao hawana vipato vikubwa” alisema Waziri Mkuu.
Aidha,
ameagiza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayeshughulikia Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa George Simbachawene na Waziri wa Ujenzi
, Uchukuzi, na Mawasiliano pamoja na wadau wakutane kupanga upya
viwango hivyo na kama watashindwa basi Serikali itaendesha mradi
huo.
Tarehe
25, Novemba 2015, Waziri Mkuu alimuagiza aliyekuwa Katibu Mkuu
Wizara ya TAMISEMI na waendeshaji wa mradi wa mabasi yaendayo kasi
Dar es salaam (UDART) kupitia misuada yote na kurekebisha miundombinu
ili mradi huo wa mabasi uanze kufanya kazi ifikapo tarehe 10,
Januari 2016, imebainika kwamba UDART hawakuandaa mpango wa biashara
wala kuanisha gharama za uendeshaji.
No comments:
Post a Comment