Breaking News
recent

WANANCHI WATAKIWA KUUNDA KAMATI ZA ULINZI SHIRIKISHI KATIKA MITAA YAO

Watanzania watakiwa kuunda na kusimamia bila ya kuoneana kamati maalum za ulinzi shirikishi ambazo watakubaliana kuziunda kwa lengo la kusimamia usalama katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam, na Kaimu Kamishna wa kanda maalum ya Dar es Salaam Simon Siro nakuongeza kuwa Jeshi la Police tayari limejipanga kushirikiana na wananchi kuhakikisha usalama wa watanzania na mali zao unazingatiwa.
    Kaimu Kamishna wa kanda maalum ya Dar es Salaam Simon Siro

Amesema Jeshi la Police kwa sasa linafanya uchunguzi kwa baadhi ya Askari wanaokiuka taratibu za kazi katika kutoa huduma kwa watanzania kama kuwaonea kwa kuwapiga bila kuzingatia haki za binadamu, kuwasingizia kesi na kulipizia kisasi wananchi.
gmbongo tha entertainer

gmbongo tha entertainer

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.