Serikali
ya Tanzania imesema pamoja na kuzingatia amani inakuwepo katika nchi
za Afrika Mashariki lakini pia itasimamia kupunguza makali ya Soko la
Huria kwa nchi hizo ili kukuza uchumi wa Wananchi wake.
Akiongea
na Waandishi wa Hbari Jijini Dar es Salaam Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt.
Augustine Mahiga amesema kupunguza makali hayo kutafanya kila
mwananchi afaidike na Jumuiya hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga
Waziri
Mahiga amesema kuwa kwa Mujibu wa Takwimu zinaonyesha kuwa Tanzania
baada ya Miaka mitano ijayo itakua ni katika nchi zenye uchumi wa
kati lakini kunatakiwa kuwepo uwiano wa Maisha katika ukuaji wa
Uchumi huo.
Waziri
Mahiga ameongeza kuwa pamoja na takwimu hizo kuonyesha hivyo lazima
tanznia ifanye juhudi za makusudi kuwatoa wananchi wake kutoka pale
walipo na kuelekea katika uchumi huo wa kati.
Aidha
Dkt. Mahiga amesema katika kuingia katika soko hilo ni lazima nchi
izingatie viwango bora vya bidhaa ambazo nchi itazalisha huku
akisisitiza kuwa nchi itatoka kwenye kuuza malighafi na kuanza kuuza
bidhaa zenyewe.
No comments:
Post a Comment