Wakati
serikali ikihimiza suala la kilimo kwanza na uwekezaji katika sekta
ya kilimo nchini kuweza kuwakwamua wananchi na umaskini, bado tatizo
la mfumo wa upatikanaji wa ardhi limeendelea kulalamikiwa kuwa tatizo
linalofanya jitihada hizo kukwama katika maeneo mbalimbali nchini
hususani mkoani Lindi.
Hayo
yamebanishwa na mwakilishi wa Mwekezaji kutoka nchini Ufaransa wa
kampuni ya Cassava Starch of Tanzania Corporation LTD,.ambao
wameshindwa kufanyia kazi azma yao ya kuanzisha kiwanda cha
kutengeneza wanga katika eneo la Mtama, kitakachokwenda sambamba na
ulimaji na ununuzi wa zao la mhogo ikiwemo kutoka kwa wakulima,kwa
madai hali hiyo inasababishwa namlolongo mrefu wa mfumo wa
upatikanaji wa ardhi,
Akitolea
ufafanuzi suala hilo Mkuu wa mkoa wa Lindi Jordan Rugimbana ,amekiri
mfumo uliopo kukwamisha hali hiyo ingawa maeneo mengi yapo wazi kwa
shughuli za kilimo na uwekezaji, na kwamba kwa sasa ameanza kufanyia
kazi hali hiyo kwa kuwatambua wawekezaji wote waliopo katika mkoa
wake na kujua mahitaji yao na kile wanachofanya ambapo zoezi hilo la
kuwapatia maeneo litawashirikisha wananchi.
Mkuu wa mkoa wa Lindi Jordan Rugimbana
Takwimu
zinaonesha mkoa huo una eneo kubwa la ardhi ambalo linafaa kwa
shughuli za kilimo lakini halitumiki,huku watafiti wakiwa tayari
wamewawezesha kupata mbegu bora za aina mbalimbali kwa ajili ya
kilimo cha mhogo.
Nao
baadhi ya wananchi wa Mtama wilayani Lindi wameziomba mamlaka husika,
kuhakikisha wawekezaji hao wanapata eneo la ukubwa wa hekta 6000 kama
walivyoomba ili waanzishe kiwanda hicho cha kutengeneza wanga,na wao
waweze kunufaika kiuchumi na fursa mbalimbali zikiwemo za ajira na
maendeleo mengine.

No comments:
Post a Comment