Wazazi
na walimu wa shule za msingi katika kata ya Bunduki wilaya ya
Mvomero mkoani Morogoro wametishia kufunga shule tano zilizopo
katika kata hiyo kutokana na shule hizo kukosa walimu na idadi ya
wanafunzi ikizidi kuongezeka huku walimu wakuu wa shule hizo
wakisusia fedha zilizotolewa na serikali kusaidia mfumo wa elimu bure
kwa madai kuwa hazikidhi mahitaji.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti walimu wakuu wa shule za msingi Tandari
Maguluwe, bunduki , vinile, kibigili, wametupia lawama serikali
kushindwa kupeleka walimu wa kutosha huku shule za mijini zikiwa na
walimu zaidi ya 20 kila shul huku wao wakiwa hawafiki hata walimu
watano tu.
Nao
baadhi ya wazazi wamesema watoto wao wanahitimu darasa la saba bila
kujua kusoma na kuandika kutokana na mwalimu mmoja kufundisha watoto
zaidi ya 400 ambapo wamesema mfumo wa elimu bure kwa wanafunzi
haitakuwa na maana endapo shule hizo zitaendelea kuwa na upungufu
mkubwa wa walimu.
Akijibu
malalamiko hayo kwa njia ya simu Afisa elimu wilaya ya Mvomero bwana
Michael Ligola amesema hana mamlaka ya kuzungumzia kero hizo bali
anayetakiwa kuyajibu ni mkurugenzi wa halmashauri hiyo ambapo
jitihada za kumtafuta mkurugenzi huyo zimegonga mwamba baada ya simu
yake kutopatikana.
No comments:
Post a Comment