Waziri
wa nchi sera,uratibu na Bunge ,ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama
amewatembela na kuwafariji wwaathirika wa Majanga ya mvua
zinazoendelea kunyesha ambazo zimeharibu nyumba za wananchi na
kuwaacha bila makazi ya kuishi Mkoani Ruvuma.
Maeneo
yaliyotembelea na Waziri huyo ambae pia ni mbunge wa Pramiho Mkaoni
Ruvuma ni pamoja na kata ya magagura ambapo ametoa msaada wa shilingi
laki 9 kwa kata hiyo pamoja na kata ya Mbinga Mharule.
Akiongea
na Wakazi wa Vijiji hivyo baada ya kukumbwa na maafa hayo Bi.
Jenista ameagiza kupandwa kwa miti ili kujikinga na upepo na
kupunguza Athari za Majanga kama hayo ya Mvua.
Waziri wa nchi sera,uratibu na Bunge ,ajira na Walemavu Mh. Jenista Mhagama
Katika
matukio hayo watu kadhaa walijeruhiwa ikiwemo mama na mwanae ambao
waliangukiwa na ukuta wa Nyumba yao ambapo baadhi ya wananchi
walioathirika na maafa hayo wamehifadhiwa katika nyumba za Serikali.

No comments:
Post a Comment