Mbunge
wa jimbo la Ubungo na Mh. Said Kubenea leo amesomewa maelezeo ya
awali ya tuhuma za kutumia lugha za matusi dhidi ya mkuu wa wilaya ya
kinondoni Paul Makonda.
Akisoma
maelezo hayo ya awali mbele ya hakimu mkazi mkuu, Thomas Simba wa
mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakili wa
serikali Mutalemwa Kisheni amesema kuwa mnamo tarehe14/12/2015 maeneo
ya Mabibo Jijini Dar es salaam katika kiwanda cha Tooku Garmet co.
ltd Said Kubenea alitoa lugha za matusi dhidi ya mkuu wa wilaya ya
kinondoni wakati alipokwenda kuwasikiliza wafanyakazi wa kiwanda.
Saed Kubenea (mwenye shati jeusi kulia), akizungumza jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (mwenye t-shirt ya michirizi),
Hakimu
Thomas Simba amehairisha kesi hiyo ya ambayo imefunguliwa kwa hati ya
makosa ya jinai mpaka tarehe 20 na 21 January 2016 ambapo upande wa
mashtaka wataanza kutoa ushahidi dhidi ya mtuhumiwa.
No comments:
Post a Comment