Kufuatia
kukithiri kwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ikiwemo kupigwa na
kunyanyaswa na kunyimwa fursa ya kupata elimu ,baraza la Watoto
wilaya ya Arusha limeiomba serikali ichukue hatua kali dhidi ya
watakao bainika, ili kukomesha vitendo hivyo.
Hayo
yameelezwa katika Baraza la watoto la wilaya ya Arusha lilokutana
kujadili masuala mbalimbali ikiwemo haki za watoto ,Mjumbe wa Baraza
hilo Hassan Kimaro amesema kuwa ili kuwa na taifa bora lenye ustawi
ni vyema kukemea vitendo vya kikatili kwa watoto ili visigeuke
desturi na kuathiri maendeleo ya taifa
Mwenyekiti
wa Baraza hilo Dominic Raphael na Mjumbe wa Baraza hilo Brina
Salvatory amesema kuwa kwa sasa wamejikita katika kutetea haki za
hususan wale wanaofichwa majumbani na kuhakikisha kuwa wanafichuliwa
ili waweze kupata haki zao za msingi ikiwemo elimu na mlo bora
MWENYEKITI WA BARAZA LA WATOTO ARUSHA DOMINIC RAPHAEL
Mratibu
wa wanawake na watoto jiji la Arusha ,Saumu Kweka amesema kuwa Baraza
hilo la watoto limesaidia kufichua vitendo vya kikatili dhidi ya
watoto na kuziwezesha mamlaka husika kuchukua hatua kali.
Changamoto
inayowabili watoto nchini ni pamoja na matukio ya kikatili
wanayofanyiwa majumbani ambayo asilmia kubwa hayaripotiwi katika
vyombo vya sheria ,suala linalofanya ukatili wa kijinsia kukosa
mwarobaini wa kisheria ambao unaweza kukomesha vitendo hivyo.
No comments:
Post a Comment