Serikali
mkoani Tanga imeanza kuchukua hatua za kudhibiti uharibifu wa
mazingiza unaofanywa na wafanyabiashara.
Uharibifu
huo unafanywa na wafanyabiashara wa Tanzania kwa kuashirikiana na
wafanyabiashra kutoka Kenya kwa miti aina ya Mikarambati na Mikoko
wilayani Mkinga.
Akiongelea
uharibifu huo Afisa Misitu wa Wilaya hiyo Frank Chambo amesema miti
ya mikoko imekuwa ikikatwa kwa ajili ya nishati huku Mikarambati
ikitumiwa kwa ajili ya kuchonga vinyago na wafanyabiashara kutoka
Kenya.
AKizungumza
na ITV wilayani mkinga baada ya operesheni iliyofanywa awali
kufanikiwa lakini baadhi ya wahamiaji kutoka nchi jirani ya kenya
wameanza kuingia kupitia njia za majini na njia za panya Mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi na usalama Mboni Mgaza amesema hatua hiyo
inafuatia misitu ya hifadhi kuharibiwa vibaya katika baadhi ya maeneo
na kupoteza uoto wa asili.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Mboni Mgaza

No comments:
Post a Comment