Mamlaka
ya mawasiliano nchini (TCRA), imewapa onyo kali pamoja na kuyapiga
faini makampuni matano ya kutoa huduma za mawasiliano ya simu hapa
nchini kwa kushindwa kuwalinda wateja wake.
Akitangaza
hukumu hiyo leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Dkt.
Ally Simba amesema makampuni hayo yatalipa million 25 kila moja kwa
kosa la kushindwa kuwalinda wateja wake na kusababisha matapeli
kutumia makampuni yako kuwachukulia fedha wateja kwa udanganyifu
kupitia huduma zao za kifedha.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt.Ally Yahaya Simba
Dkt.
Simba ameongeza kuwa faini hiyo italipwa mara moja na kama mamlaka
ikipokea malalamiko zaidi toka kwa wananchi Mamlaka itawachukulia
hatua kali zaidi kwa mujibu wa sheria.
Kwa
upande wa Mwanasheri wa (TCRA), bi. Elizabeth Nzagi amewataka
wananchi kuwa waangalifu pindi wanapoombwa msaada wa fedha na ndugu
zao kwa kuhakikisha kuwa wanaowaomba fedha ni ndugu zao na sio
vinginevyo.
No comments:
Post a Comment