Watu
wawili wamefariki na wengine 21 kujeruhiwa baada ya basi la abiria la
Luwinzo lililokuwa likitokea Njombe kwenda Dar es Salaam kugonga
lori, katika eneo la Mafinga, wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Akiongea
na East Africa Radio Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhan
Mungi amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa basi lililotaka
ku over-take lori hilo lakini kukawa na gari nyingine mbele jambo
lililopelekea dereva kuepusha basi lake kugongana uso kwa uso na
badala yake kuliparamia lori hilo.
Kamanda
Mungi amesema watu waliofariki katika ajali hiyo wote ni Watumishi wa
gari hilo Mmoja akiwa ni Kondakta na mwengine ni msimamizi na
kuongeza kuwa mpaka wanawashikilia maderva wa magari yote mawili kwa
ajili ya Uchunguzi Zaidi.

No comments:
Post a Comment