Bunge
la Afrika Mashariki (EALA) sasa limeamua kujitosa rasmi kusuluhisha
mgogoro wa kisiasa nchini Burundi, baada ya Asasi za kiraia na
Taasisi mbalimbali zilizoko nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika
Mashariki(EAC), kuomba Bunge hilo kuingilia kati mgogoro huo na
kuutatua.
Asasi
na Taasisi hizo ziliandika maombi yao kwa Kamati ya Bunge hilo,
inayoshughulikia migogoro na usuluhishi, ambao leo itaanza
kusikiliza hadharani maombi yao, kwa siku tatu mfululizo na baadaye
itapeleka mapendekezo katika Bunge hilo, kwa ajili ya kulitolitolea
azimio
Akizungumza
jana na waandishi wa habari jijini kwenye ofisi za Bunge hilo,
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Abdullah Ali Hassan Mwinyi amesema,
wananchi wenye nafasi na kuguswa na suala hilo, wanakaribishwa
kushiriki katika mhadhara huo, ambao utawasilisha maoni ya wananchi
juu ya mgogoro huo wa Burundi.
Wabunge wa Tanzania kwenye bunge la Afrika Mashariki(EALA)wakitoka ndani ya ukumbi wa bunge hilo
Mwinyi
amesema katika mhadhara huo, asasi hizo za kiraia na Taasisi
zitawasilisha hoja mbalimbali za kulitaka Bunge hilo, kuingilia kati
mgogoro huo na kwamba mapendekezo yatakayowasilishwa Bungeni,
yatakuwa sehemu ya
mkakati
wa kusuluhisha mgogoro huo.
Amesema
wao kama Bunge wajibu wao kusikiliza pande zote, katika mgogoro huo
ikiwa
ni pamoja na wananchi, vyama vya kiraia na kijamii,upinzani na hata
serikali,
ili kuwa katika mazingira mazuri ya kuelewa kiini cha mgogoro na
kutoa
mapendekezo stahili, yatakayomaliza mgogoro huo.
Amezitaja
asasi hizo na baadhi ya Taasisi zilizowasilisha maombi kuwa
ni
pamoja na Chama cha Wanasheria wa Afrika (PALU),Asasi ya Haki za
Binadamu ya Attrocities Watch Afrika,Kituo cha Ushiriki wa wananchi
wa Afrika katika Umoja wa Afrika,Chama cha Wanasheria wa Afrika
Mashariki na Kituo cha Katiba.
Burundi
imekuwa katika mgogoro wa kisiasa tangu Rais Pierre Nkurunziza
alipotangaza
nia ya kuongeza muhula wa tatu wa uongozi wake mapema mwaka
jana,
hatua iliyopingwa vikali na vyama vya upinzani nchini humo.
Licha
ya kupingwa,Rais Nkurunzinza ameendelea na nia yake na kufanya
uchaguzi
uliosusiwa na upinzani na kutangazwa kuwa mshindi huku mauaji ya
raia
yakiendelea hasa baada ya jaribio la kumpindua kushindikana.
Mauaji
hayo yamesababisha raia wengi wa nchi hiyo, kuikimbia nchi yao na
kusababisha
mtafaruku wa mapambano kati ya majeshi ya serikali na waasi
ambao
wamekuwa wakipambana katika mji mkuu wa Bujumbura nchini humo.

No comments:
Post a Comment