Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed
Shein amesema kuwa hatua za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Awamu
ya Saba za kuimarisha huduma za afya za vijijini ni miongoni mwa
utekelezaji wa shabaha ya Mapinduzi ya mwaka 1964 ya kuzifikisha
huduma bora za afya hadi vijijini kwa nia ile ile ya waasisi wa
Mapinduzi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
Dk.
Shein aliyasema hayo katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba na
Waziri wa Nchi Afisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dk. Mwinyi Makame
Mwadini, mara baada ya kulifungua jengo la wagonjwa wa nje katika
Hospitali ya Kivunge, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Katika
hotuba hiyo, Dk. Shein alisema kuwa huduma bora za afya kwa wananchi
wote bila ya ubaguzi ni miongoni mwa malengo ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar ya mwaka 1964 ambapo Chama cha ASP kilichoongoza Mapinduzi
hayo katika manifesto yake, kiliweka bayana azma yake ya kutoa huduma
za afya bure bila ya ubaguzi wakati kitakaposhika hatamu za Serikali.
Dk.
Shein alisema kuwa jitihada kubwa zimefanywa na Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar katika kipindi cha miaka 52 ya Mapinduzi katika
kuimarisha huduma za afya kwa kutambua kwamba afya bora ni muhimu kwa
wananchi ili waweze kuishi vyema katika kazi ya kuleta maendeleo ya
nchi yao.
Alisema
kuwa mafanikio makubwa yamepatikana katika utekelezaji wa mipango na
mikakati ya kuiendeleza sekta ya afya nchini kupitia vitengo na
programu mbali mbali zinazoendeleshwa na Serikali kwa ushirkiano na
Washirika wa Maendeleo.

No comments:
Post a Comment