Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema watu waliojenga mabondeni
wanaobomolewa nyumba zao hawatalipwa fidia ikiwemo kupewa viwanja na
kuonya kuacha kuvamia mashamba ya watu kwa kuwa hatua kali za
kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam Mkuu huyo wa Mkoa Bw,
Meck Sadick amesema kuwa wakazi hao wa mambondeni wanapaswa kuondoka
wenyewe wasibiri fidia ambayo haipo.
MWENYEKITI wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Dar es Salaam, ambaye pia ni Mkuu wa mkoa huo, Saidi Mecky Sadik
Meck
Sadick amesema hayo huku zoezi la Bomoa bomoa likiwa linaendelea
katika maeneo ya Mkwajuni huku akisisitiza kuwa zoezi hilo linafanywa
kwa mujibu wa sheria ya mazingira ambayo inawataka wananchi wasijenge
katika maeneo hatarishi.
Aidha
Mkuu huyo wa Mkoa amesisitiza kuwa zoezi hilo sio la Dar es Salaam
peke yake kama wengi wanavyodhani bali ni la nchi nzima na
litaendelea kwa kadiri siku zinavyokwenda.

No comments:
Post a Comment