Waziri
Mkuu wa Tanzania Kassimu Majaliwa amesema kuwa hakuna Mtanzania
atakayekufa kwa njaa kwa kuwa serikali ina akiba ya chakula cha
kutosha kwenye maghala yake.
Aidha
amesema kuwa kazi iliyopo hivi sasa kwa serikali ni ya kugawa na
kupeleka chakula hicho kwenye maeneo yote yenye mahitaji ikiwemo
maeneo yaliyokumbwa na mafuriko.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo alipofanya ziara ya kutembelea kijiji cha
Majeleko kilichopo wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma ambacho ni
miongoni mwa vijiji vilivyoathirika na njaa na kuwalazimu wananchi
kuishi kwa kula matunda aina ya zambarau na baadhi ya wadudu.
Waziri
Mkuu amesema bado kuna akiba nzuri ya chakula ambacho kitasambazwa
maeneo yote yenye mahitaji nchini.
Aidha
amewataka wananchi kuacha kutumia chakula cha msaada kwa ajili ya
kupikia pombe na kila mmoja awe askari wa mwenzake na watakaobainika
kufanya hivyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
No comments:
Post a Comment