Halmashauri
ya Bagamoyo Mkoani Pwani inaongoza nchi nzima kwa udanganyifu wa
uuzwaji wa ardhi kwa watu binafsi,kughushi Muhtsari ya majina pamoja
na kutumia ardhi kukopea mabalioni ya fedha kwa maslahi binafsi.
Akizungumza
na Watendaji wilayani Bagamoyo katika ziara yake ya kikazi waziri wa
Ardhi, Nyumba na maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema kuwa
kuanzia sasa utaratibu wa uuzwaji wa ardhi ubadilishwe na
kuwashirikisha wakuu wa wilaya.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
Mhe.
Lukuvu ameongeza kuwa Wilaya hiyo inaongoza kwa kughushi kutokana na
kuwa na mikutano mingi feki ikiwa ni pamoja na watu kuuziana Ardhi
jijini Dar es Salaam na kupelekea copy tu za mikataba ambayo
haijakidhi viwango vya uuzwaji.
Akiwa
wilayani humo Mhe. Lukuvi alitembelea amsjara ya ardhi na kuvumbua
madudu ikiwemo ucheweleshwaji wa hati za viwanja kwa watu wasiokuwa
na kipato huku matajiri wakiharakishiwa huduma hiyo huku baadhi ya
watendaji wakishindwa kutimiza wajibu wao.
Wakielezea
matatizo wanayokutana nao vijijini hapo katika mkutano wao wake wa
hadhara wananchi wengi wamesema kuwa wamekua wanadhurumiwa ardhi zao
ikiwemo uuzwaji wa viwanja hivyo bila ridhaa yao huku wengine
wakitishiwa.

No comments:
Post a Comment