Mama
mmoja Mkoani Dodoma anatuhumiwa kumuozesha mtoto wake mwenye umri wa
miaka 13 (jina linahifadhiwa) kwa mahari ya shilingi laki sita pamoja
na ng’ombe wanne.
Tukio
hilo lilitokea jana katika Mtaa wa Chikole, Kata ya Msalato katika
Manispaa ya Dodoma ambapo mama huyo aliyefahamika kwa jina la Melea
Mazengo ameamua kumuozesha binti yake huyo kwa kijana mmoja
aliyefahamika kwa jina moja la Juma ambaye naye ni mkazi wa mtaa
huo.
Hata
hivyo mpango huo wa ndoa ulitibuliwa na mwenyekiti wa mtaa huo,
Nashoni Chinywa ambaye baada ya kupata taarifa za ndoa hiyo aliamua
kuita polisi ili kuivunja.
Akizungumzia
tukio hilo mama mzazi wa mtoto huyo, Mdala Mazengo amesema kuwa
aliamua kumuozesha binti yake baada ya binti huyo kumtaarifu kuwa
amepata mchumba.
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Watoto Ummy Mwalimuakitoa changamoto kwa wasichana kutilia mkazo Elimu badala ya kujihusisha na vitendo vya mapenzi
Kwa
upande wa binti huyo amesema kuwa alikutana na kijana huyo Juma (20)
na kumwambia kuwa anampenda lakini yeye aliona kuwa anamtania na
kuamua kuachana naye.
Hata
hivyo baadhi ya majirani wa mama huyo wamesema kuwa ni tabia ya mama
huyo ambaye ni mjane kuwaozesha watoto wake wakiwa katika umri mdogo
kwani kuna mwanaye mmoja mwenye umri wa miaka 14 alibebeshwa mimba na
mpaka sasa ana mtoto mdogo anayemlea.
Insert
shuhuda
Naye
mwenyekiti wa mtaa huo, Nashoni Chinywa amesema kuwa baada ya
mahojiano mama huyo alikiri kosa lake na kusema kuwa amechochwa na
malezi ya watoto hao kwani hata dada yake mwenye umri wa miaka 14
alibebeshwa mimba akiwa nyumbani hivyo akaona ni bora amuozeshe na
huyo mdogo wake ili asije akabeba mimba nyumbani.

No comments:
Post a Comment