Waziri
wa nchi ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora
Mhe. Anjela Kairuki amesema kuwa mawaziri wakuu wastaafu wanahaki
yakuendelea kuhudumiwa na serikali kwa mujibu wa hitimisho la kazi
namba 3 ya mwaka 1999 na kuendelea kupewa stahiki zao kwa mujibu wa
sheria ya nchi inavyoelekeza.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Mhe. Anjela Kairuki
Waziri
Kairuki ameyasema hayo leo mjini Dodoma wakati akijibu swali la
Mbunge wa Dimani mhe. Hafidhi Ali Tahir ambaye alitaka ufafanuzi
mawaziri wakuu wastaafu kujihusisha na siasa wakati huohuo bado
wanahudumiwa na serikali na kuitaka sheria hiyo ifanyiwe marekebisho.
Waziri
Kairuki amesema kuwa mawaziri wakuu wastafu wanahaki ya kujiunga na
chama chochote au kujihusisha na masuala ya kisiasa kwakua ni haki
yao kikatiba na haki hizo haziwezi kuingiliwa.
Wakati
huohuo Waziri Kairuki amekemea tabia ya watumishi wa serikali ambao
wanahudumia jamii kwa kubagua matabaka ya vyama kuwataka waache mara
moja na watekeleze sera za serikali kwa kutambua kuwa nchi inamfumo
wa vyama vingi.

No comments:
Post a Comment