Vijana
kote nchini wametakiwa kuachana na matumizi ya madawa ya kulevya
pamoja unywaji wa pombe uliopitiliza kwani unywaji huo unaathiri afya
zao na kuteketeza nguvu kazi ya taifa pamoja na kuchochea maovu
katika jamii ikiwemo,wizi,ubakaji na ukatili wa kijinsia.
Hayo
yameelezwa na Mchungaji wa Kanisa la Anglican Church ,Cannon Kajembe
katika ibada ya mazishi ya mtoto wa mtaani maarufu kama watoto wa
dampo aliyefariki baada ya kupigwa na wananchi wenye hasira kali kwa
kuhusishwa na uporaji wa simu ya mkononi.
Mchungaji wa Kanisa la Anglican Church ,Cannon Kajembe
Kajembe
amewataka vijana kutumia nguvu zao kujenga jamii na taifa badala
kujihusisha na matendo yasiyofaa huku akiitaka serikali iwachukulie
hatua wauzaji wa pombe maarufu kama viroba .
Hata
hivyo Mkurugenzi wa Kampuni ya madini ya Thom Gems,Thomas Munisi
aliyejitokeza kusaidia ibada ya mazishi ya mtoto huyo wa mtaani
,amelitaka jeshi la polisi kuwachukulia hatua watu waliohusika na
tukio hilo la mauaji kwani walijichukulia sheria mikononi hadi kutoa
uhai wa kijana huyo ambaye mwili wake ulijeruhiwa vibaya kwa kipigo
kikali hadi kifo.
Kwa
upande wake Redman Joseph ambaye ni Mtoto wa mtaani na rafiki wa
marehemu ameitaka jamii na serikali kuchukua hatua kuwasaidia watoto
wa mitaani na kuwaendeleza ili kuepuka kujiingiza kwenye makundi
mabaya ambayo huatarisha maisha yao na jamii kwa ujumla.
Mwili
wa kijana Maiko Massawe aliefariki januari 22 umepumzishwa kwao
maeneo ya Kibosho wilaya ya Moshi mkoa wa Kilimanjaro,Serikali,jamii
na watu binafsi hawana budi kuwasaidia watoto wa mitaani ili kuokoa
maisha yao na ndoto zinazopotea.
No comments:
Post a Comment