Mwalimu
wa shule ya Msingi Ikombohinga iliyopo wilayani Chamwino Mkoani
Dodoma, Peter Hema, amechapwa makofi na Ofisa elimu wa hiyo Mohamed
Msongo kwa kosa la kuchelewa kufika kwenye semina ya kufundisha
watoto stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK).
Tukio
hilo lilitokea baada ya mwalimu huyo kuchelewa kufika kwenye mafunzo
hayo kwa takribani dakika 40 kwani alitakiwa kufika saa 2:00 lakini
alifika saa 2:40 yeye pamoja na wenzake kwenye semina hiyo yenye
lengo la kuwajengea watoto wa darasa la kwanza na la pili stadi za
kusoma kuandika na kuhesabu.
Akielezea
sakata hilo mwalimu alipigwa Peter Hema alisema kuwa Ofisa elimu
huyo amemdhalilisha kwa kumpiga kibao baada ya kuchelewa kufika
kwenye semina hiyo waliyokuwa wakiifanya.
Waziri wa Elimu,Sayansi, Teknolojia na Ufundi Pro. Joyce Ndalichako
Kufuatia
hali hiyo mwenyekiti Chama Cha walimu Wilaya ya Chamwino (CWT)
Clementi Mahenga alisema kuwa chama hicho kinalaani vikali tukio hilo
na kuitaka serikali kuhakikisha inamchukulia hatua kali za kisheria
Ofisa elimu huyo kwa kukiuka kanuni na sheria za utumishi wa umma.
Alisema
baadhi ya viongozi wamekuwa wakiitumia vibaya kaulimbiu ya Hapa kazi
tu kwa kuwadhalilisha na kuwaonea watumishi wa ngazi za chini
serikalini.
Alipotafutwa
Ofisa elimu huyo ili kuzungumzia tuhuma hizo alikanusha vikali kuwa
yeye hakumpiga vibao wala hakumsukuma mwalimu huyo.
Kwa
upande wake Kaimu mkurugenzi wa Chamwino Richard Masimba alipotafutwa
ofisini kwake alisema taarifa hizo hawana na watazifuatilia.
Masimba
alisema ofisi haina taarifa ya mwalimu kupigwa vibao na kusukumwa
ukutani na iwapo itathibitika hatua za kisheria na kinidhamu
zitachukuliwa dhidi ya Ofisa Elimu huyo.

No comments:
Post a Comment