Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvivu, Mwigulu Nchemba amewanusuru wanachama wa
vyama vya ushirika wa kilimo cha Tumbaku wilayani Iringa kutapeliwa
na baadhi ya viongozi wao, matrekta tisa yaliyokopeshwa kwa vyama
hivyo kupitia mkopo uliotolewa na benki ya CRDB, miaka minne
iliyopita.
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvivu, Mwigulu Nchemba
Ameamuru
viongozi hao tisa kutoka chama cha ushirika Mfyome, Magubike, Kiwemu,
Kitai, Mhanga na Kampuni ya umoja wa Wakulima wa Tumbaku Iringa
(ITCOJE Ltd) wakabadhi ofisi zao mara bada ya kuondoka Iringa jana.
Pamoja
na kuwataka viongozi hao waachie ngazi na taratibu za kujaza nafasi
zao zifanywe haraka iwezekanavyo, Waziri Nchemba amemuagiza Mrajisi
wa Vyama vya Ushirika nchini, Dk Audax Lutabazibwa kuifuta bodi ya
ITCOJE na kuhakikisha taratibu za kuunda bodi mpya zinafanywa haraka
iwezekanavyo.
Mbali
na kumiliki gari la kisasa aina ya Toyota Land Cruiser VX bodi hiyo
pia inamiliki roli aina ya Scania linalofanya kazi ya kusambaza kuni
na pembejeo kwa wanachama wa vyama hivyo
Nchemba
alikuwepo mjini Iringa juzi kwa mwaliko wa wakulima wa Tumbaku wa
wilaya ya Iringa ambao pamoja na mambo mengi yanayohusu changamoto za
kilimo na biashara ya tumbaku nchini, walimueleza jinsi baadhi ya
viongozi wao wanavyotumia madaraka yao kujineemesha kinyemela kupitia
mgongo wa vyama hivyo.
Kati
ya watuhumiwa hao tisa yupo Mwenyekiti wa ITCOJE, Msafiri Pamagila na
Afisa Ushirika wa Wilaya ya Iringa, Emanuel Samile ambaye waziri huyo
ametaka achunguzwe kama alizingatia taratibu za kazi na sheria
zinazounda vyama hivyo wakati naye akinufaika na moja ya matrekta
hayo.
Kabla
ya kutoa maamuzi hayo, Nchemba alitumia takribani saa 4 kuwasikiliza
walalamikaji (wanachama wa vyama hivyo) na walalamikiwa (viongozi
watuhumiwa) na kujiridhisha kwamba viongozi hao walitumia madaraka
yao kufanya udanganyifu uliolenga kuwahalalishia umiliki wa matrekata
hayo ambayo mkopo wake ulilipwa na wanachama wa vyama hivyo.
Akitumbua
majipu, Nchemba aliyembatana na Lutabazibwa na Mkurugenzi wa Bodi ya
Tumbaku Tanzania, Wilfred Mushi katika kikao kilichofanyika katika
ukumbi wa siasa ni kilimo baina yake na wakulima wao alisema:
“Mkuu
wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa na vyombo vyenu nitamke hapa hapa kwamba
matrekta hayo ni mali ya vyama vya msingi, kwa kuwa yalikopeshwa
kupitia vyama hivyo na yamelipwa na wanachama wenyewe kupitia vyama
vyao vyao vya msingi kama ambavyo ushahidi kutoka CRDB unaonesha.
Mkurugenzi
wa CRDB Iringa, Kisa Samwel alikiri katika kikao hicho kuvikopesha
vyama hivyo mkopo uliotumika kununua matrekta hayo kwa kupitia
mwavuli wao wa ITCOJE na wala mikopo hiyo haikuwa kwa ajili ya
viongozi wanaotajwa.
“Nikuhakikishie
mheshimiwa waziri, benki yetu ilikopesha vyama na mikataba inaonesha
hivyo; haya madai ya mikopo hiyo kugeukwa ya viongozi fulani
hatuyafahamu na hayatuhusu. Kwetu sisi wakopaji ambao ni vyama ndio
waliolipa mikopo hiyo na mpaka sasa nyaraka zinaonesha hivyo,”
alisema.
Alisema
mikopo ya matrekata hayo ilikwishalipwa na vyama hivyo lakini
yameendelea kutumika kama dhamana katika benki hiyo baada ya vyama
hivyo kuyatumia kukopa fedha kwa ajili ya msimu wa kilimo wa
2015/2016 unaonendelea.
Awali
mmoja wa wanachama wa vyama hivyo, Ombeni Mvella alimwambia waziri
kwamba inashangaza matrekata hayo ambayo mkopo wake ulilipwa na
vyama hivyo, kumilikishwa kwa watu wachache kiunjaunja.
“Mheshimiwa
waziri tunanyanyaswa na viongozi wa ITCOJE, tulidhani ni watetezi wa
wakulima, sasa wameguka kuwa wanyanyasaji wa vyama vya msingi,’.
Matrekata yalikopeshwa na vyama lakini yemeguka kuwa mali ya viongozi
wachache,” alisema.
Katika
utetezi wao, watuhumiwa hao walisema waliteuliwa na wanachama wa
vyama hivyo kuwa wasimamizi wa matrekta hayo kwa makubaliano kwamba
watayamiliki moja kwa moja baada ya mikopo yake kwisha; jambo
lililomshangaza waziri na viongozi wengine waliokuwepo.
“Yaani
kwa kuwa msimamizi tu basi mali husika inageuka kuwa yako. Kwahiyo na
mimi nikisimamia wizara hii itakuwa sahihi kweli baada ya miaka
mitano nipewe rachi moja au kingine chochote ambacho ni mali ya
umma?” aliuliza kwa mshangao.
Akijitetea,
Mwenyekiti wa ITCOJE alisema; “katika makubaliano yaliyotuwezesha
kunufaika na matrekata haya hata sisi tulikuwa tukilipa fedha zetu.
Mimi binafsi nililipa Sh Milioni 7 ili kupata trekta hilo ambalo pia
nimekuwa nikilitumia kwa gharama zangu kulima mashamba ya wanachama
wa vyama vya msingi.”
Naye
Afisa Ushirika wa wilaya ya Iringa, Samile alijitetea akisema alipata
trekta analomiki kwa kuwa yeye ni mmoja wa wanachama wa vyama hivyo
vya ushirika mwenye mashamba makubwa.
“Nikiri
kwamba trekta langu nimelipata kwa kupitia mkataba wa kulisimamia
kama ilivyo kwa wengine. Sijatoa hata senti tano katika mkopo wake na
niseme wazi kwamba matrekta hayo yalikopeshwa kwa vyama vya msingi,
sisi sio wakopaji wala walipaji; sisi tumepewa baada ya kuyasimamia,”
alisema huku akitetemeka.

No comments:
Post a Comment