Waziri
wa Kilimo, mifugo na Uvivu, Mhe. Mwigulu Nchembe amewafukuza kazi
Mkuu wa mnada wa Pugu na watumishi waliokuwa zamu kuanzia tare 24
mwezi 12 mwaka jana hadi tarehe 1 mwaka huu kutokana na kuwepo kwa
ubadhirifu wa ukwepaji kodi.
Akiongea
leo Jijini Dar es Salaam baada ya kufanya ziara na Mawaziri wengine
wawili Akiwemo wa TAMISEMI,Mhe. Nchemba amesema kuanzia sasa watafute
kazi nyigine,na wahakikishe wanafika ofisi ya Katibu mkuu wizara ya
mfiguo mapema Jumatatu tar.04/01/2016.
Mhe. Mwigulu Nchemba, Mhe George Simbachawene na Mhe. Hamis Kigwangala wakiteta jambo
Aidha
Waziri huyo amesema kuanzia sasa serikali imesitisha uchukuaji wa
Ushuru eneo la mnada wa pugu,badala yake makusanyo yote ya fedha za
serikali hizo yatafanyika Machinjio ya Vingunguti kwa kutumia mashine
za Elektroniki za EFD,na mnada wa pugu utakuwa unatumika kutoa vibali
tu vya mifugo ilikudhibiti ubora wa mifugo inayopaswa kuchinjwa.
Katika
hatua nyingine amesema kuwa eneo la kuhifadhia nyama lililokuwa
limejengwa kwa fedha za Wananchi kushirikiana na serikali lifunguliwe
kwaajili ya Wananchi kulitumia kuhifadhia nyama hiyo,Awali eneo hilo
lilifungwa bila sababu za msingi.
Aidha
Mh. Mwigulu amesema kuwa umeme uliokuwa umekatwa eneo hilo urudishwe
hii leo kwa ajili ya kuwarahisishia wananchi shughuli zao huku akiita
Halmashauri ya ilala kuboresha miundombinu ya Machinjio hayo.
Kwa
upande wake Naibu waziri wa afya jinsia , watoto na wazee Dkt. Hamis
Kigwangala amewataka Madaktari waliokuwa na jukumu la kuthibitisha
mifugo hiyo kama inafaa kwa matumizi ya binaadamu kupisha uchunguzi
kwani kumeonekana kuwepo na wanyama wasiofaa kuliwa na binaadamu
machinjioni hapo


No comments:
Post a Comment