Serikali
imeanza kurejesha ardhi kubwa ambayo baadhi ya watu waliimiliki kwa
muda mrefu bila kuiendeleza huku wananchi wengi wakikosa ardhi kwa
ajili ya kufanyia maendeleo.
Waziri
wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi ametoa
agizo la Hekta 1800 za Ardhi katika Shamba la Kapunga, Katika Kijiji
cha Kapunga Wilayani mbalali Mkoani Mbeya zirejeshwe kwa Wananchi
baada ya muwekezaji aliepewa ardhi hiyo kushindwa kuiendeleza.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mh. William Lukuvi
Akiongea
na Wanakijiji wa kijiji hicho katika Mkutano wa Hadhara Waziri
Lukuvi amesema kwa rais alivyoagiza wakati wa kampeni zake kwa wale
walioshindwa kuendeleza Ardhi na kushindwa kuiendeleza basi
itarejeshwa kwa wananchi wa eneo husika kwa ajili ya kufanya
Maendeleo.
Waziri
Lukuvi baada ya kusikiliza kero za Wananchi wa Kijiji cha Kapinga
amesema Rais Magufuli ameamua kuzirejsha kwa Wananchi hekta hizo 1800, baada ya mmiliki ya shamba la Kapunga Estate
kumilikishwa kimakosa.
No comments:
Post a Comment