Mamlaka
ya chakula na dawa nchini TFDA imeamua kuanzisha mfumo maalumu wa
kutathmini magonjwa yanayotokana na ulaji wa vyakula visivyo salama
na njia za kukabiliana na magonjwa hayo kwani vyakula hivyo
vimetajwa kuchangia kwa kiasi kikubwa magonjwa yanayosumbua
binaadamu.
Akiongea
na kurasa Meneja mahusiano wa TFDA Gaudensia Simwanza amesema kuwa
kwa muda mrefu sasa Tanzania inakabiliwa na changamoto ya kukosekana
kwa takwimu sahihi na kwa wakati zinazohusu magonjwa yanayosababishwa
na ulaji wa vyakula visivyosalama hivyo kuchelewesha kupatikana njia
za kutatua matatizo hayo..
Meneja mahusiano wa TFDA Gaudensia Simwanza
Akiyataja
baadhi ya magonjwa yatokanayo na ulaji wa vyakula visivyo na ubora ni
pamoja na kansa ya ini, magonjwa ya figo , magonjwa ya kuhara damu,
homa ya matumbo, minyoo na amiba.
Aidha
amewataka wanachi kuzingatia kanuni za afya wakati wa kuzalisha mazao
ya chakula , uhifadhi wa chakula ,uaaandaaji wa chakula na ulaji wa
vyakula kwani wakati mwingine chakula kinaweza kikazalishwa kwa
kufuata kanuni za afya lakini vikahifadhiwa kwa madawa ambayo
yanakemikali za sumu na hatari kwa afya ya binaadamu.

No comments:
Post a Comment