Serikali
imesema kuwa tayari imekwisha peleka fedha kwenye wilaya zote
Tanzania bara na tayari wameshawapa wakuu wa mikoa, wilaya na
wakurugenzi na kuwataka kuhakikisha wanazisimamia fedha hizo ziende
moja kwa moja kwenye mashule husika bila ucheleweshwaji ili zianze
kutumika.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa nchini
TAMISEMI Mhe. George SimbaChawene leo Jijini Dar es Salaama
alipoongea na East Afrika radio na kusema fedha hizo ni kwa ajili ya
gharama walizokua wanatoa wazazi kwa shule za msingi na Sekondari
nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa nchini TAMISEMI Mhe. George SimbaChawene
Simbachawene
ameongeza kuwa fedha hizo zinatolewa kwenye mashule kulingana na
idadi ya wananfunzi iliyonayo ikiwa ni pamoja na fedha za uendeshaji
wa shule,fidia ya ada,fidia kwajili ya mitihani na chakula kwa ajili
ya shule za bweni.
NEWS
CLIP
Aidha
Mhe. Simbachawene amekemea baadhi ya wakuu wa shule kuendelea kuwadai
wazazi fedha kwa kisingizio cha wao kutoshirikishwa kwenye jambo hilo
na kuwataka wazazi kuendelea kuchangia michango mbalimbali.
No comments:
Post a Comment