Baadhi
ya viongozi wa siasa nchini wametaka wigo wa mazungungumzo ya mgogoro
wa kisiasa visiwani Zanzibari upanuliwe kwa kushirikisha wadau wote
baada ya kuviachia vyama vinavyovutana vya CCM na CUF peke yao.
Akizungumza
na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa chama cha
NCCR-Mageuzi Mhe. James Mbatia ametaka mgogoro huo kutatulia kwa
mujibu wa katiba ya Zanzibar pamoja na kuhusisha kituo cha demokrasia
nchini ili kupata suluhusu ya suala hilo.
Mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi Mhe. James Mbatia
Mhe.
Mbatia amesema kuwa mgogoro huo wa kikatiba usipotatuliwa na
kuwafuata busara ya kuwahusisha wadau tofauti unaweza kusababisha
machafuko visiwani humo na kuliharibia jina taifa pamoja na kugharimu
maisha ya watanzania.
Kwa
upande wake Makamu mwenyekiti wa chama cha sauti ya Umma (SAU),Bw.
Yusuph Manyanga amesema kuwa majadiliano ya vyama viwili kwa sasa
hayalengi kutafuta suluhisho kutokana na kila chama kuvutia upande
wake.

No comments:
Post a Comment