Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha kusindika tumbaku cha
mkoani Ruvuma na kuwasimamisha kazi viongozi wa Chama Cha Kikuu Cha
Ushirika cha SONAMCU.
Akizungumza
jana jioni(Jumanne, Januari 5, 2016), katika ukumbi wa mikutano wa
Ikulu Ndogo ya Songea, wakati alipokutana na wakulima wa zao la
tumbaku wa Wilaya ya Namtumbo, Wananchama wa Vyama Vya Ushirika vya
Mkoa wa Ruvuma, viongozi wa Mkoa pamoja na Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Edwin Ngonyani ambaye ni Mbunge wa Jimbo la
Tunduru Kaskazini.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Waziri
Mkuu amesema, Serikali ina dhamira ya kufufua kiwanda cha kusindika
tumbaku cha SONAMCU, na lengo la kutembelea kiwanda hicho ni katika
utekelezaji wa agizo la Rais John Pombe Magufuli la kufufua viwanda
nchini.
Waziri
Mkuu Majaliwa, ametembelea maeneno mbalimbali ya kiwanda hicho na
kukagua mitambo iliyokua ikitumika kusindika tumbaku, kabla kiwanda
hicho kuzimwa miaka kadhaa iliyopita baada ya kukosa malighafi za
kuendelea na uzalishaji.
Pia,
amemtaka Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara Bibi.
Stela Lugongo kuandaa na kuwasilisha kwake mkakati wa kufufua kiwanda
hicho cha kusindika tumbaku, na baadae kuwasimamisha kazi viongozi
wote wa Chama Kikuu cha Ushirika cha SONAMCU waliohusika na tuhuma
hizo na kutaka wafikishwe Mahakamani.
“Serikali
imeazimia kufufua viwanda, hasa vile ambavyo havina wawekezaji
vimebaki vyenyewe, Tunahitaji kujua namna ya kuvifufua”. Alisema
Waziri Mkuu huku akishangiliwa.
Waziri
Mkuu Majaliwa pia, amesikiliza na kujibu kero mbalimbali za wakulima
wa tumbaku wa Mkoa huo, ambao walilalamikia mfumo wa Vyama vya
Ushirika na namna ambavyo vyama hivi vimekua vikiwaibia fedha zao
hadi kushindwa kuendelea kulima zao la tumbaku na kukosa masoko ya
mazao yao.
Aidha,
Waziri Mkuu amewasihi wakulima kuwa watulivu na kusubiri maamuzi ya
Mahakama baada ya kuwa viongozi wa Chama cha Ushirika SONAMCU ambao
wamehusika na wizi wa fedha za wakulima kiashi cha Shilingi milioni
800 kwa kipindi cha mwaka 2011 hadi 2014 tayari wamefikishwa
Mahakamani na uchunguzi unaendelea. Pia, amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma Said Thabit Mwambungu kukutana na wakulima hao ili kupatia
ufumbuzi matatizo yao.
Aidha,
ametoa wito kwa wakulima kuendelea kulima zao la tumbaku kwa kuwa
linaongeza pato la mtu mmoja mmoja, linasaidia kuchangia pato la Mkoa
na kukua kwa uchumi wa nchi. Amewashauri wakulima kuunda na
kuviendesha Vyama Vya Ushirika kwa kuzingatia sheria, kanuni na
taratibu zilizopo.
Waziri
Mkuu amemaliza ziara yake mkoani Ruvuma, atafanya majumuisho ya ziara
hiyo leo, kabla ya kuagana na viongozi wa Chama na Serikali na
kurejea jijini Dar es Salaam.

No comments:
Post a Comment