Shirika
la Afya Duniani, WHO limesema kesho litaitisha mkutano maalum kuhusu
kirusi aina ya Zika ambapo kirusi hicho tayari kimeripotiwa kwenye
nchi 20 huku Brazil ikiwa ni nchi iliyoathirika zaidi.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo mjini Geneva, msemaji wa WHO Christian
Lindmeier ameeleza kwamba kirusi chenyewe cha Zika si hatari, kwani
huhasababisha tu ukurutu mwilini.
Msemaji wa WHO Christian Lindmeier
Hata
hivyo ameeleza kwamba Brazil imeshuhudia pia visa 4,000 vya watoto
wanaozaliwa na vichwa vidogo, miongoni mwao 49 wakiwa wamefariki
dunia, ikidaiwa hali hiyo kuwa na uhusiano na kirusi cha Zika.
Aidha
amesema kwamba WHO haijapendekeza wanawake kujikinga dhidi ya kupata
mimba, akieleza kwamba suluhu dhidi ya kirusi cha Zika hivi sasa ni
kujikinga na mbu aina ya Aedes, ikiwa ni Brazil au kwingineko.
No comments:
Post a Comment