Naibu
waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamadi Masauni ameitaka idara
ya uhamiaji nchini kuwasaka, kuwakamata, kuwashtaki na kuwarudisha
makwao raia wote wa kigeni wanaoishi bila vibali halali vya kuishi na
kufanyakazi hapa nchini.
Naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Hamadi Masauni
Naibu
waziri Masauni amesema kuwa wageni wote wanaonyanyasa watanzania
katika makampuni yao washughulikiwe haraka na wale wanaofanya kazi
zinazoweza kufanywa na wazawa waondolewe nchini ili watanzania wapate
hizo ajira.
Aidha
masauni ameongeza kuwa idara ya uhamiaji itaanzisha mahakama yake ya
kijeshi ili maafisa wasio waaminifu na wala rushwa washughulikiwe
haraka ILI kuleta uadilifu katika sekta hiyo,
Wakati
huo huo Kamishina wa uhamiaji wa mkoa wa Dar es Salaam John Msumule
amesema wanatarajia kukamata wageni 350 katika kampeni inayoanza leo
japo kuna changamoto ya uchache wa watumishi pamoja na vitendea kazi
kama magari na fedha za kuwasarifisha wale watakaotakiwa kurudishwa
nchini mwao.
No comments:
Post a Comment