Watu
11 wafariki dunia wakiwemo madereva wote wawili na mtoto mmoja wa
umri wa miaka miwili na wengine 29 kujeruhiwa baada ya basi la abiria
la Simba mtoto lilokuwa likitokea Jijini Tanga kuelekea jijini Dar
es Salaam kupata ajali kwa kugongana na lori katika Mkoani Tanga.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Tanga Mihayo Msikhela amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kusema kuwa imetokea katika kijiji cha Pangamlima
Barabara ya Tanga-Segera wilayani Muheza na kuongeza kuwa kati ya
majeruhi wawili kati yao hali zao ni mbaya
Akielezea
Chanzo cha Ajali hiyo Kamanda Mskhlea amesema kuwa ni uzembe wa Derva
wa lori ajali ambae inasemekana alisinzia na kuhama upande wake na
kuhamia upande mwingine wa barabara na kusababisha magari hayo
kugongana uso kwa uso.
Kamanda
Msikhela amesema kati ya watu walifariki dunia sita wamekwisha
tambuliwa akiwemo mtoto wa miaka miwili huku akiongeza kati ya vifo
Wanaume ni nane na wanawake ni watatu akiwemo na mtoto huyo wote
wakiwa ni wa familia moja
No comments:
Post a Comment