Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amelitaka jeshi las polisi nchini
kurejesha kitengo cha ulinzi bandarini na pia eneo lililokuwa
linafungwa mita za mafuta litakua linalindwa na polisi.
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue, imesema raisi magufuli ametaka jeshi la polisi
nchini kurejesha ulinzi kama ilivyokuwa nyakati za nyuma kabla
mamalka ya bandari haijaamua kubandilisha mfumo wa kuweka walinzi
wake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
Balozi Ombeni Sefue ameongeza kuwa
katika eneo ambalo linafungwa mita za mafuta (Flowmeters),ambalo
waziri mkuu alitembelea na kumisimamisha wakala mkuu wa vipimo sasa
ni lazima lilindwe na jeshi la polisi.
Aidha katika hatua nyingine Rais
Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi watatu ambao Vituo vya
uwakilishi kwa mabalozi hawa vitajulikana baada ya taratibu husika za
kidiplomasia kukamilika huku akiwateua makamishna wa jeshi la Polisi.

No comments:
Post a Comment