Mbunge wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA), wa jimbo la Kawe na Madiwani wawili wa chama
hicho jana walihojiwa na polisi kutokana na vurugu zilizotokea katika
uchaguzi wa Meya wa Jiji na hivyo kuahirishwa.
Jana Mchana Mbunge huyo wa Kawe
aliwasili katika kituo kikuu cha Polisi akiongozana na Mbunge wa
Bunda Mhe. Esther Bulayo ambapo waliingia katika kituo hicho na kukaa
kwa masaa kadhaa ambapo hakukuwa na taarifa kamili ya mahojiano hayo
yalihusiana na nini.
Halima mdee akizozana na polisi mara baada ya kuingizwa kwenye gari
Aidha madiwani wawili waliohojiwa na
polisi wa kata za Mbezi na Salanga pamoja na Kada mmoja wa Chama
hicho ambae hakuweza kufahamika mara moja nafasi yake ambapo wote
walishikiliwa na jeshi hilo kutokana na tuhuma za kuhusishwa na
vurugu hizo.
Aidha Jeshi la Polisi limesema kuwa
linaendelea kumtafuta Mbunge wa Ukonga kwa tiketi ya CHADEMA, Mhe.
Mwita Waitara kwa mahojiano zaidi kutokana n a vurugu hizo.
Uchaguzi wa Meya wa Dar es Salaam
ulihairishwa siku ya Jumamosi baada ya katibu tawala wa Mkoa wa Dar
es Salaam Therisia Mbando kutangaza kutofanyika uchaguzi huo kutokana
na zuio la Mahakama.
No comments:
Post a Comment