Serikali imesema hairidhishwi hata
kidogo na utendaji kazi unaofanywa na wakala wa serikali wa
umeme na ufundi Temesa katika uendeshaji wa shughuli za vivuko
nchini pamoja na ukusanyaji wa mapato.
Akizungumza na wafanyakazi wa
wizara ya ujenzi,uchukuzi na mawasiliano mkoani mara, waziri
wa wizara hiyo mhe. Prof Makame Mbarawa,amesema katik siku za
hivi karibuni serikali italazimika kuchukua uamuzi mgumu hasa
kwa kufanya mabadiliko ya watendaji wote wa wakala huyo ili
kuongeza uwajibikaji.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa
Katika mkutano huo waziri huyo
amesema serikali pia imepanga kutumia dola milioni 3o kwa
ajili ya matengenezo na ukarabati mkubwa wa uwanja wa ndege wa
Musoma mkoani Mara.
Amesema hatua hiyo imelenga
kuwaondolea kero wanayoipata wananchi wa mkoa wa Mara
wakiwemo watalii wanaofika mkoani humo kabla kutembelea hifadhi
ya taifa ya Serengeti ikiwa ni njia moja wapo ya kumuenzi baba wa
taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Kuhusu kampuni ya simu nchini
TTCL,waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Mh. ameitaka
kampuni hiyo kuacha ukilitimba kwa kuitegemea serikali katika
kufanya biashara hiyo na kwamba wanapaswa kuongeza wateja na
katika kukuza ukusanyaji wa pato la taifa.
No comments:
Post a Comment