Watu tisa wamepoteza maisha na
wengine 473 wameugua ugonjwa wa kipindupindu katika kipindi cha wiki
moja toka February 22 hadi 28 mwaka huu huku Mkoa wa mara ukitajwa
kuongoza kwa maambukizi mapya ya Ugojwa huo.
Akiongea na Waandishi wa Habari jana
Jijini Dar es Salaam Naibu Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto,Dkt. Khamis Kigwangala amesema licha ya
jitihada za serikali kutokomeza ugonjwa huo lakini bado kuna baadhi
ya wataalamu wa Afya pamoja na Wanajamii wanaendelea kuwa chanzo cha
kuenea kwa ugonjwa huo.
Naibu Waziri wa afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Dkt. Khamis Kigwangala
Mhe. Kingwala amesema wkumekuwepo
na tabia ya Wataalamu hao wa Afya pamoja na Wanajamii kuficha
wagonjwa pamoja na kutoa taarifa ya wagonjwa wachache kuliko uhalisia
kunakwamisha juhudi za serikali kutokomeza ugonjwa huo.
Naibu Waziri huyo ametumia fursa
hiyo kuzitaka mamlaka husika kutoka taarifa sahihi za wagonjwa ili
kurahisisha njia za kupambana na ugonjwa huo ambao umeripotia karibu
mikoa yote ya Nchini Tanzania.
Aidha amewataka viongozi wa Mikoa na
Wilaya kuto kutoa kauli za kuwatisha wataalamu wa Afya na viongozi wa
ngazi za chini kwa kigezo cha wagonjwa wa kipindupindu kwa ni kwa
kufanya hivyo wataongeza kasi ya jamii kuwaficha wagonjwa wa
kipindipindu.
No comments:
Post a Comment