Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto ndio yenye dhamana ya kusimamia huduma za
afya kwa wananchi imesema itaendelea kutoa taarifa za mara kwa mara
kwa wananchi kuhusu milipuko ya magonjwa ikiwamo kipindupindu.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Ummy Mwalimu
Taarifa hiyo iliyotolewa kwa vyombo
vya habari imewataka Viongozi wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha
upatikanaji wa taarifa sahihi, mapema kwa kuzingatia miongozo na kwa
wakati bila kuficha pindi wanapopata wagonjwa wapya.
Pia taarifa hiyo imeeleza kuwa
jamii isiwekewe vikwazo vya faini au kunyanyapaliwa wapatapo ugonjwa
huu kwani inaweza kusababisha wananchi kuogopa kwenda katika vituo
vya afya.
Aidha imewataka Wakuu wa Mikoa na
Wilaya wawasiliane na Wizara iwapo kuna ufafanuzi wowote unaohitajika
kwa taarifa zinazotolewa kuhusu magonjwa hayo ya mlipuko.

No comments:
Post a Comment