Mamlaka
ya bandari(TPA), imezisimamisha kazi kampuni 210 za uwakala wa kutoa
mizigo bandarini kutokana na kushindwa kuwasilisha vielelezo vya
malipo waliyoyafanya wakati wa kutoa mizigo.
Kampuni
hizo zinatuhumiwa kuhusika kutorosha makontena 11,884 na Magari 2019
kutoka bandari kavu(ICD), saba za jijini Dar es Salaam bila kulipiwa
ushuru wa bandari,hibyo kuipotezea serikali mapato ya shilingi
bilioni 48.
Meneja wa mawasiliano wa TPA, Janet Ruzangi
Meneja
wa mawasiliano wa TPA, Janet Ruzangi amesema hayo jana na kusema kuwa
mawakala hao wamesimamishwa baada ya kupewa muda wa kuwasilisha
nyaraka hizo mwishoni mwa Desemba mwaka jana Kushindwa.
Ruzagi
amesema mawakala hao 210 ni kati ya mawakala 280 ambao waziri mbarawa
aliwataka kuwasiliosha nyaraka za malipo sahihi kwa mizigo ambayo
waliiondoa ndani ya bandari hiyo kuanzia julai hadi desemba mwaka
jana.
Katika
maelezo yake Menejea huyo mawasiliano amesema mara baada ya kampuni
hizo za uwakala wa forodha zitakapowasilishwa vielelezo hivyo vya
malipo bandari itawafungulia na kuendelea kufanya nao biashara.
No comments:
Post a Comment