Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt.
Jakaya Kikwete amemshurukuru raisi Magufuli kwa kumteua kuwa mkuu wa
chuo na kuahidi kuendeleza upanuzi na uboreshaji wa chuo hicho.
Akizungumza
na viongozi mbalimbali chuoni hapo baada ya kufanya ziara Dkt.
Kikwete amesema atahakikisha chuo kikuu cha Dar es Salaam kinaendelea
kuaanda wataalamu na viongozi na viongozi wa fani mbalimbali ndani na
nje ya nchi.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete
Dkt
Kikwete alitembela vitivo mbalimbali katika chuo hicho kwa ajili ya
tafiti na maktaba zitakazowezesha chuo hicho kupokea wanafunzi wengi
zaidi ambapo kwa sasa chuo hicho kinapokea wanafunzi 22,000.
Rais
Kikwete amesema anatamani chuo hicho kiwe chuo kikubwa nchini na
Afrika kinachotoa viongozi ambapo mtu akitaka mtaalamu yoyote aweze
kufikilia kwanza muhitimu wa chuo kikuu kabla ya kufikiria kwengine.
Kwa
upande wake Makamu Mkuu wa chuo hicho Pro. Rweikaza Mukandala
amemshukuru rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kumteua Dkt. Kikwete
kuwa mkuu wa chuo hicho kutokana na mchango wake katika chuo wakati
yupo madarakani.

No comments:
Post a Comment